JUAN MATA NYOTA WA MCHEZO, LIVERPOOL NA MAN U

JUAN MATA NYOTA WA MCHEZO, LIVERPOOL NA MAN U

Like
494
0
Monday, 23 March 2015
Slider

Liverpool imeshindwa kuutumia uwanja wake wa nyumbani katika mchezo wake na klabu ya Manchester United baada ya kuruhusu kupokea kichapo cha magoli 2 kutoka kwa Manchester huku wakiambulia goli moja lakufuta machozi lilifungwa na Daniel Sturridge.

Goli la kwanza la Man U lilifungwa na Juan mata ambapo Liverpool iliamua kufanya mabadiliko kuimarisha safu yake ya ulinzi kwakumuingiza nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard kuchukua nafasi ya Adam Lalana aliyepata jeraha.

Hata hivyo nahodha huyo hakupata nafasi ya kuendelea na mchezo baada ya kulimwa kadi nyekundu kwa kufanya madhambi ya kumkanyaga Ander Herrera kadi iliyoathiri mchezo huo kwa upande wa Liverpool

Baadae Juan Mata aliitumia nafasi hiyo ya kuyumba kwa ukuta wa Liverpool kufunga goli la pili

mmm mm m4 m3 m1

Comments are closed.