MAZUNGUMZO ya kutatua mzozo unaokumba Sudan Kusini yamegonga mwamba, saa kadhaa kabla ya Umoja wa Mataifa kuwawekea vikwazo wanaohusika.
Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir na mpinzani wake ambaye aliwahi kuwa makamu wake, Riek Machar, wamekuwa wakijadili mipango ya kugawanya mamlaka ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha maelfu ya watu kuuawa na zaidi ya watu milioni moja na nusu kupoteza makazi.
Umoja wa mataifa umetishia kuwawekea vikwazo watu binafasi wanaojaribu kuzuia makubaliano hayo iwapo makundi hayo mawili hayatatia saini mwafaka kabla ya muda uliotengwa.