Jukwaa la Katiba Tanzania-JUKATA limewataka wananchi kuisoma na kuielewa Katiba iliyopendekezwa huku wakilinganisha na Rasimu ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 sanjari na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania HERBRON MWAKAGENDA amesema ili kufanikisha hilo Serikali inatakiwa iwezeshe upatikanaji wa nakala za kutosha za Katiba inayopendekezwa na Rasimu ya katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Katiba ya Tanzania na Zanzibar.