JUKWAA LA SERA NA MTANDAO WA ASASI ZA KIRAIA LAPANGA KUZUNGUMZA NA WACHIMBAJI WA MADINI

JUKWAA LA SERA NA MTANDAO WA ASASI ZA KIRAIA LAPANGA KUZUNGUMZA NA WACHIMBAJI WA MADINI

Like
271
0
Friday, 27 February 2015
Local News

JUKWAA la sera na mtandao wa asasi za kiraia unaoshughulikia maswala ya utawala bora na uwajibikaji,  umeandaa  mjadala uliojadili na kuangazia namna uchimbaji wa madini unaofanywa na makampuni na kuangalia jinsi wanavyowajibika kwa jamii, kwa wafanyakazi wanao waajiri na jinsi wanavyotunza mazingira ili kuandaa mazingira bora na kuleta maendeleo endelevu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mratibu wa jukwaa la sera Senkaye Kilonzo amesema kama asasi za kiraia zinazoangalia maswala hayo wameona kuna haja ya kukaa na kujadili na kampuni  kubwa na ndogo za madini ili kuwajengea uwelewa sawa  juu ya utunzaji wa mazingira, ukuzaji wa uchumi na maendeleo endelevu.

Comments are closed.