JUMA NATURE KUMWAGA MISAADA LEO

JUMA NATURE KUMWAGA MISAADA LEO

Like
296
0
Thursday, 28 May 2015
Entertanment

MSANII wa Muziki wa Bongo flaver nchini,  Juma Kassim Ally, maarufu Juma Nature leo anatarajiwa kutoa misaada ya vitu mbalimbali katika Hospitali ya Serikali ya Zakhiem, mbagala jijini Dar es salaam.

Akizungumza na EFM Juma nature amesema lengo la kutoa msaada huo, ni sehemu yake ya kumshukuru Mungu wakati anatimiza miaka kumi na sita tangu aanze kazi hiyo ya Muziki.

Kilele cha maadhimisho hayo ya miaka kumi na sita ya Juma Nature katika Muziki kitakwenda sambamba na hitimisho la maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kituo hiki kianze kurusha matangazo yake ambapo yatafanyika jumamosi katika Viwanja vya Dar Live mbagala jijini Dar es salaam.

Comments are closed.