JUMLA YA KINA MAMA MILIONI 1 NA LAKI 6 WANAKADIRIWA KUUGUA FISTULA NCHINI

JUMLA YA KINA MAMA MILIONI 1 NA LAKI 6 WANAKADIRIWA KUUGUA FISTULA NCHINI

Like
322
0
Tuesday, 21 April 2015
Local News

IMEELEZWA  kuwa jumla ya Kina Mama Milioni 1 na laki 6 Nchini Tanzania wanakadiriwa kuugua ugonjwa wa Fistula huku kukiwa na ongezeko la wagonjwa Wapya Elfu 3 kila mwaka wanaougua ugonjwa huo kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo  uzazi usio salama.

Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa  na CCBRT, nchini Tanzania kuhusiana na Ugonjwa huo, umeonyesha kuwa katika kipindi cha miaka 12 iliyopita Tanzania ilikadiriwa kuwa na wagonjwa Elfu 24 mpaka Elfu 30 wanaougua  ugonjwa wa Fistula huku wengi wao wakipata ugonjwa huo kutokana na Mila Potofu.

Akizungumza na EFM Meneja wa Hospitali ya CCBRT, KASPAR MMUYA amesema kuwa ugonjwa wa  Fistula ni Ugonjwa unaowapata Akina Mama Wajawazito kutokana na  nyonga zao kuonekana kutotanuka hivyo kupelekea kutokea kwa tundu katika kibofu cha mkojo hali inayopelekea kutokwa na mkojo mara kwa mara.

Comments are closed.