JUMUIYA YA VIJANA CUF IMEMTAKA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZULU

JUMUIYA YA VIJANA CUF IMEMTAKA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AJIUZULU

Like
299
0
Friday, 30 January 2015
Local News

JUMUIYA ya Vijana CUF –JUVICUF imemtaka waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe kujiuzulu kufuatia tukio la kupigwa na kudhalilishwa kwa mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba,viongozi waandamizi na wanachama wake,pamoja na kutoa kauli ya uongo bungeni jana.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa JUVICUF Hamidu Bobali amesema kuwa wanasikitishwa na vitendo vilivyofanywa na jeshi la polisi na kulaani ukimya wa viongozi wa juu pamoja na upotoshaji unaofanywa na viongozi hao pamoja na kuitaka Serikali kuzifuta kesi zinazowakabili wanacuf waliokamatwa katika kadhia hiyo.

Aidha JUVICUF imemtaka Mkuu wa jeshi la polisi IGP Ernest Mangu kutokubali wananchi kuliona jeshi hilo limekosa watu wa kujenga hoja mbele ya umma na kukanusha kauli ya Mkuu wa operesheni maalum za jeshi la polisi SSP Simon Siro kuwa sababu ya kuzuia maandamano ya cuf ni kufuatia tukio la kuporwa silaha kwa askari huko Ikwiriri.

 

Comments are closed.