JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KUFANYA USAFI MANISPAA YA ILALA

JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KUFANYA USAFI MANISPAA YA ILALA

Like
418
0
Tuesday, 08 December 2015
Local News

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Tanzania inatarajia kufanya usafi wa Mazingira katika baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Ilala ikiwa ni hatua ya kuunga mkono Agizo la Rais Dokta John Pombe Joseph Magufuli la kufanya usafi siku hiyo.

Akizungumza  na Wanahbari jijini Dar es salaam Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Jeddah Hasabubaba amewataka Wafanyabiashara wote wa Jumuiya hiyo kujitokeza na kushiriki kufanya usafi wa mazingira.

Aidha Hasabubaba ameongeza kuwa suala hilo halitokuwa suala la siku moja bali ni endelevu na kuwa wanaunga mkono agizo hilo  na wanaipongeza  Serikali ya awamu ya tano kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa na Wananchi.

Comments are closed.