JWTZ YAKANUSHA KUPELEKA MAJESHI ZANZIBAR

JWTZ YAKANUSHA KUPELEKA MAJESHI ZANZIBAR

Like
328
0
Thursday, 17 March 2016
Local News

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekanusha taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi cha uchaguzi wa marudio unaotarajia kufanyika Machi 20 mwaka huu.

 

Jeshi hilo limesema kuwa Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma kwani JWTZ lina Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa Taifa hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu awali.

 

Comments are closed.