KADCO YAOKOA BILIONI MBILI KWA KUZUIA WIZI WA NYARA ZA SERIKALI

KADCO YAOKOA BILIONI MBILI KWA KUZUIA WIZI WA NYARA ZA SERIKALI

Like
261
0
Wednesday, 23 December 2015
Local News

KAMPUNI ya maendeleo ya viwanja vya ndege –KADCO,  inayosimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) imesema imeokoa zaidi ya kiasi cha shilingi  Bilioni  mbili katika kipindi cha wiki moja ikiwa ni thamani ya nyara za serikali na vito vya thamani vilivyokuwa vitoroshwe kupitia uwanja huo.

 

Menejimenti ya uwanja huo kupitia kitengo cha usalama ilifanikiwa kukamata vipande 264 vya madini ya Tanzanite vikiwa na uzito wa kilograamu 2.04 ambavyo thamani yake inakadiriwa kufikia Bilioni 2.5.

 

Kwa mujibu wa Kaimu mkurugenzi wa KADCO, Bakari Murusuri Desemba 18 ,maofisa usalama uwanjani hapo walimkamata abiria mwenye asili ya Uarabuni akiwa na pembe mbili za Twiga.

IMG_2170 (1024x683)

Comments are closed.