KAKA SUNGURA AVAMIWA NA MAJAMBAZI

KAKA SUNGURA AVAMIWA NA MAJAMBAZI

Like
223
0
Tuesday, 26 May 2015
Entertanment

Mastar wengi na watu maarufu barani Afrika hivi karibuni wamekuwa wakizionyesha silaha zao kwenye mitandao ya kijamii ambazo wengi wao haifahamiki kama wanamili kisheria au la.

Lakini pia inawezekana wanafanya hivyo kama njia ya kujihami kufuatia kuongezeka kwa matukio ya uharifu wa kutumia silaha.

Star wa muziki kutokea Kenya kaka sungura mwishoni mwa wiki iliyopita alivamiwa na watu aliodai kuwa ni majambazi waliokuwa na silaha na kumuibia laptop yake aina HP Envy 17 pamoja na simu yake mpya aliyonunua wiki moja iliyopita wakati yupo hotelini na mtu wake wakaribu wakifanya mazungumzo.

Star huyo aliongeza kuwa majambazi hao hawakuficha nyuso zao na walifanya tukio hilo kwakumpitia kila mtu aliekuwa akipata chakula hotelini hapo

Zaidi kaka sungura amewaomba wasamalia wema kupatia data zilizomo kwenye laptop hiyo kwani ni muhimu zaidi kwake lakini ametuma kipande cha video kilichorekodiwa na Camera za ulinzi hotelini hapo wakati tukio hilo linaendelea

 

https://youtu.be/uNgYBMvi2j8

Comments are closed.