KAMANDA WA POLISI MKOANI ARUSHA AKANUSHA TAARIFA ILIYOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO JUU YA KUKAMATWA KWA MTU ANAESADIKIKA KUWA GAIDI

KAMANDA WA POLISI MKOANI ARUSHA AKANUSHA TAARIFA ILIYOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO JUU YA KUKAMATWA KWA MTU ANAESADIKIKA KUWA GAIDI

Like
241
0
Friday, 10 April 2015
Local News

KAMANDA wa Polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabasi, amekanusha taarifa zilizoenea leo katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kukamatwa kwa mtu mmoja aliyevalia vazi la baibui akiwa na bomu Mkoani humo na kusema habari hizo siyo za kweli na ni uzushi.

Mapema asubuhi ya leo kumekuwepo na taarifa ziliyoenezwa kwenye mitandao ya kijamii zikisema kuwa Maafisa wa Usalama Mkoani Arusha usiku wa kuamkia leo wamekama gari aina ya Toyota Premio nyeusi ikiwa na watu wanne na bunduki nne aina ya SMG na risasi 160 wakiwa wanajaribu kuingia Chuo cha Uhasibu Arusha-IAA.

Hata hivyo taarifa za kiusalama kutoka IAA zinasema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kwamba wananchi wanaombwa kuzipuuza.

Comments are closed.