KAMATI TEULE YA BUNGE YAITAKA SERIAKALI KUBORESHA NA KUIMALISHA MABARAZA YA ARDHI

KAMATI TEULE YA BUNGE YAITAKA SERIAKALI KUBORESHA NA KUIMALISHA MABARAZA YA ARDHI

Like
275
0
Friday, 06 February 2015
Local News

KATIKA kupambana na migogoro ya Ardhi kati ya Wakulima,Wafugaji na Wawekezaji Kamati teule ya Bunge imeitaka serikali kufanya maboresho na kuimarisha  Mabaraza ya Ardhi ili kuwe na wataalam wenye sifa zinazokidhi mahitaji ya usuluhishi wa migogoro hiyo.

Mapendekezo hayo yametolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Mjumbe wa Kamati teule ya bunge alipokuwa akisoma ripoti ya kamati hiyo iliyoundwa kuchunguza na kutafuta njia  za kutatua migogoro hiyo CHRISTOPHER OLE SENDEKA ambapo ameitaka serikali iimarishe mabaraza hayo katika ngazi ya vijiji, Kata na Wilaya  kwa kutatua changamoto mbali mbali zinazoyakabili mabaraza hayo ikiwemo ile ya watendaji wenye weledi na vitendea kazi.

 

Comments are closed.