KAMATI YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI YARIDHISHWA NA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAJI RUFIJI MKOANI PWANI

KAMATI YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI YARIDHISHWA NA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAJI RUFIJI MKOANI PWANI

Like
482
0
Wednesday, 21 January 2015
Local News

KAMATI ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeeleza kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji ya Kibiti na Ikwiriri iliyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani kutokana na kuonesha mafanikio makubwa.

Hayo yamesemwa na Kiongozi wa Wajumbe wa Kamati hiyo Amina Makilagi, Mbunge, baada ya kukagua miradi hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji Tanzania Bara inayofanywa na baadhi ya wajumbe wa kamati katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Mradi wa Kibiti wenye visiwa virefu vitano vinavyozalisha maji safi na salama, huzalisha meta za ujazo 55 kwa saa huku ule wa Ikwiriri ukiwa na kisima kirefu chenye urefu wa meta 60 na kipenyo cha 14 cha ujazo na una matanki mawili yenye uwezo wa mita za ujazo 500 kila moja.

MAJ3 MAJ5 MAJI MAJI2

Comments are closed.