KAMATI Ndogo ya maadili ya Chama cha Mapinduzi – CCM, leo inakutana kwa lengo la kuanza kazi ya kuwachunguza makada wake wakiwemo wajumbe wa NEC na Kamati kuu.
Hatua ya kuanza kuchunguza kwa makada wa chama hicho hususani waliotuhumiwa kwenye sakata la Tegeta Escrow, ni utekelezaji wa agizo la Kamati Kuu ya CCM, iliyokutana Visiwani Zanzibar kujadili masuala mbalimbali wiki iliyopita.
Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, amesema vikao vya kamati hiyo vitaanza leo na kasha kuchukua hatua stahiki za kinidhamu iwapo itabainika kuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni na taratibu za chama.