KAMBI RASMI YA UPINZANI KUISHAURI SERIKALI KUWASILISHA MISWADA KWA MFUMO WA KAWAIDA

KAMBI RASMI YA UPINZANI KUISHAURI SERIKALI KUWASILISHA MISWADA KWA MFUMO WA KAWAIDA

Like
201
0
Thursday, 26 March 2015
Local News

KAMBI Rasmi ya Upinzani imesema  italifanyia kazi ombi lililowasilishwa na wadau mbalimbali, kuitaka Kambi hiyo,kuishauri Serikali kuwasilisha Miswada kwa mfumo wa kawaida na Si kwa hati ya dharura.

Kauli hiyo imekuja Siku moja baada ya wadau,kuomba Serikali ishauriwe kuwasilisha Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari na Muswada wa Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2015,chini ya mfumo wa kawaida.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari jijini Dar es salaam,na Mbunge wa jimbo la Ubungo,JOHN MNYIKA kwa niaba ya Kiongozi wa Kambi hiyo,imeeleza kuwa imekubali ombi hilo na kuahidi kutoa ushauri huo kwa Serikali na kusimamia utekelezaji wake.

Comments are closed.