KAMPUNI ILIYOPEWA TENDA YA KUKUSANYA UCHAFU UPANGA MAGHARIBI KUVUNJIWA MKATABA

KAMPUNI ILIYOPEWA TENDA YA KUKUSANYA UCHAFU UPANGA MAGHARIBI KUVUNJIWA MKATABA

Like
438
0
Wednesday, 30 December 2015
Local News

KUFUATIA kukithiri kwa uchafu katika kata ya Upanga Magharibi licha ya kuwepo kwa kampuni ya TIRIMA iliyochukuwa tenda ya kufanya usafi katika kata hiyo,  Uongozi  umekusudia kuvunja mkataba na kampuni hiyo.

 

Diwani wa kata ya Upanga Magharibi Adinani Kitwana Kondo amesema eneo lililopo hospitali ya Muhimbili limekithiri kwa uchafu kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya watu wengi wanaoishi na wanaotembelea maeneo hayo.

 

Kondo  amesema  kampuni hiyo  ya TIRIMA imekuwa ikikusanya shilingi elfu kumi na tano kwa kila mkazi wa eneo la Upanga bila kutekeleza wajibu huo wa kufanya usafi jambo ambalo amesema ni sawa na kuwatapeli wananchi  hivyo hakuna sababu ya kuendelea kufanya kazi na kampuni hiyo.

Comments are closed.