KAMPUNI YA APPLE YATANGAZA KUPINGA AMRI YA MAHAKAMA

KAMPUNI YA APPLE YATANGAZA KUPINGA AMRI YA MAHAKAMA

Like
289
0
Wednesday, 17 February 2016
Local News

KAMPUNI ya Apple imesema itapinga amri ya mahakama ya kuwasaidia wachunguzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani FBI kuchukua habari katika simu ya muuaji wa watu 14 katika eneo la San Bernadinho nchini Marekani.

 

Kampuni hiyo ilikuwa imeamrishwa kulisaidia shirika hilo la FBI kuifungua simu ya aina ya iphone ya Farook Syed ambayo wanasema ina habari muhimu.

 

Katika taarifa yake mkurugenzi mkuu wa Apple Tim Cook amesema Serikali ya Marekani inaitaka Apple Kuchukua hatua kama hizo ambazo zinatishia usalama wa wateja wake.

Comments are closed.