KAMPUNI YA HALOTEL YATOA HUDUMA BURE KWA TAASISI ZA SERIKALI BABATI

KAMPUNI YA HALOTEL YATOA HUDUMA BURE KWA TAASISI ZA SERIKALI BABATI

Like
497
0
Monday, 19 October 2015
Local News

BAADHI ya Taasisi za Serikali ikiwemo hospitali na shule kadhaa za Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, zimepatiwa bure huduma ya mtandao wa simu mpya ya kampuni ya Halotel kwa ajili ya kuwarahisishia wapate huduma bora.

Akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi wa mtandao huo, Meneja wa Halotel Mkoa wa Manyara Adolf Kiwale amesema kuwa wameweka mitandao ya intanenti bure kwa taasisi hizo muhimu ili kurahisisha kazi zao.

Amesema licha ya kuzisaidia taasisi hizo wataendelea kutoa misaada kwenye taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali ili wajiweke karibu na wateja wao.

Comments are closed.