KAMPUNI ZINAZOTUMIA MITANDAO ZIMETAKIWA KULINDA TAARIFA ZAO

KAMPUNI ZINAZOTUMIA MITANDAO ZIMETAKIWA KULINDA TAARIFA ZAO

Like
212
0
Tuesday, 11 August 2015
Local News

KUTOKANA na ongezeko la uhalifu katika mitandao ya kijamii, kampuni mbalimbali nchini zinazojihusisha na shughuli zake kwa kutumia Mitandao zimetakiwa kuongeza umakini katika kulinda taarifa zao dhidi ya watumiaji wabaya wa mitandao hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano uliowakutanisha wataalamu mbalimbali wanaoshughulika na mifumo ya k ompyuta, mtendaji mkuu wa wakala wa serekali mtandao Dokta GABRIEL BAKARI amesema kuwa sekta ya teknolojia inakuwa kwa kasi nchini hivyo ni vyema tahadhari za kulinda mitandao hiyo zikachukuliwa mapema.

Naye Mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano tanzania –TCRA- dokta ALLY SIMBA amebainisha kuwa mamlaka hiyo kwa kushirikiana na jeshi la polisi itahakikisha kuwa yeyote atakayesambaza  taarifa za uchochezi hasa  kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi  mkuu atachukuliwa sheria.

Comments are closed.