Kanisa kongwe la Notre-Dame lateketea Ufaransa

Kanisa kongwe la Notre-Dame lateketea Ufaransa

1
837
0
Tuesday, 16 April 2019
Global News

Moto mkubwa umezuka katika kanisa kongwe la Notre-Dame mjini Paris Ufaransa ambalo ni moja ya makanisa maarufu na linalotembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka pande mbali mbali duniani kila mwaka.

Vikosi vya zima moto vinaendelea kuzima moto huo katika kanisa hilo lililodumu kwa takriban miaka 850.

Sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo yameteketezwa na mto huo huku moto katika minara miwili ya kengele umefanikiwa kuzimwa.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana, lakini maafisa maafisa wanauhusisha mkasa huo na shughuli ya ukarabati inayoendelea.

Wazima moto wanafanya kila juhudi kuokoa vito vya thamani vilivyoko ndani kanisa hilo na pia kuzuia mnara wa upande wa kasskazini kutoporomoka.

Maelfu ya watu wamekusanyika katika barabara zilizo karibu na kanisa hilo kushuhudia mkasa huo wakiwa kimya.

Baadhi yao walionekana wakidondokwa na machozi, huku wengine wakiimba nyimbo za sifa na kuomomba Mungu.

Makanisa kadha nchini Ufarasa yamekua yakipiga kengele kuashiria uharibifu wa moto huo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron,ambaye alifika katika eneo la tukio amesema mawazo yake yako na “waumini wote wa kanisa katoliki na wafaransa wote kwa ujumla.”

“Sawa na watu wengine nchini , nimesikitika sana kuona sehemu ya maisha yetu ya kila siku ikiteketea.”

Bw. Macron awali alifutilia mbali hutuba mmuhimu kwa taifa kufuatia moto huo, alisema afisa wa Élysée Palace.

Msemaji wa kanisa hilo pia amekiri kuwa sehemu kubwa imeteketea na bado inaendelea “kuteketea”.

Mwanhistoria Camille Pascalameliambia shirika la habari lla Ufaransa BFMTV kwamba moto umeharibu ”turathi ya kitaifa”

“Kanisa hili limedumu Paris kwa takribani miaka 800 “, alisema.

“Matukio ya furaha na ya kusikitisha kwa karne kadhaa yamekua yakiadhimishwa kupitia mlio wa kengele za Notre Dame.

“Tunasikitishwa na kile kilichotokea na kile tunachojionea”.

Meya wa jiji la Paris, Anne Hidalgo ametoa wito kwa wakaazi kuheshimu mipaka iliyowekwa na maafisa wa zima motoili kuwahakikishia usalam wao.

“Kuna kazi nyingi inayoendelea ndani …hili ni janga kubwa,” aliwaambia wanahabari.

The Notre-Dame cathedral, ambalo umaarufu wake huwavuvia maelfu ya watalii kila mwaka, lilikua likifanyiwa ukarabati baada ya nyufa zake kupasuka na kuzua hofu huenda jengo hilo likawa dhaifu.

Mwak jana, kanisa katoliki liliomba msaada Ufaransa kufanyia ukarabati jengo la kanisa hilo la zamani.

Maelezo kuhusu Notre-Dame

  • Kanisa hilo hupokea karibu wageni milioni 13 kila mwaka, idadi ambao ni kubwa kuliko watalii wanaozuru Eiffel Tower
  • Lilijengwa katika karne ya 12 na 13 na limekuwa likifanyiwa ukarabati mkubwa.
  • Sanamu kadhaa ziliondolewa kanisani hapo ili kuruhusu ukarabati wake.
  • Palaa la lanisa hilo lililoteketezwa na moto lilikua limetengenezwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mbao

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *