KANSELA ANGELA MERKEL AMESEMA SERIKALI YAKE ITATUMIA NJIA ZOTE KUPAMBANA NA UBAGUZI

KANSELA ANGELA MERKEL AMESEMA SERIKALI YAKE ITATUMIA NJIA ZOTE KUPAMBANA NA UBAGUZI

Like
219
0
Wednesday, 14 January 2015
Global News

SIKU  baada ya kuuita Uislamu kuwa ni sehemu ya Ujerumani, Kansela ANGELA MERKEL amesema serikali yake itatumia njia zote ilizonazo kupambana na ukosefu wa uvumilivu na ubaguzi, akitaja kutoshirikishwa kwa baadhi ya makundi ya kijamii kuwa ni jambo la kulaumiwa.

Matamshi yake yamekuja siku moja baada ya waandamanaji 25,000 wanaoupinga Uisilamu kuandamana katika mji wa Mashariki wa Dresden kutaka sheria kali zaidi za uhamiaji na kukomesha sera ya kukubali utamaduni mbalimbali.

Comments are closed.