KATANGA ATEULIWA KUWA AFISA HABARI WA DRFA

KATANGA ATEULIWA KUWA AFISA HABARI WA DRFA

Like
333
0
Wednesday, 21 January 2015
Slider

Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA jana kilimtangaza Mwandishi na mtangazaji wa Habari za michezo kutoka kwenye kituo hiki cha

EFM kwenye dawati la michezo la E sport Omary Katanga kuwa msemaji Mpya wa chama hicho.

Katanga anachukuwa nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mohamed Mharizo ambae amekubaliana na uongozi kuachia nafasi hiyo.

Katanga maarufu kama mlinda mlango namba moja ulimwenguni anawika katika medali ya utangazaji wa habari za kimichezo katika kipindi cha Esport,kinachoruka kila siku sa moja hadi saa mbili usiku, ameahidi kutopepesa macho wala kung’ata maneno katika majukumu yake.

“Nimepokea uteuzi huu kwa moyo mkunjufu kabisa”alisema Katanga “Nafasi hii ambayo nimepewa ni nafasi ngumu lakini itakuwa rahisi kama ushirikiano utatoka kwenu(waandishi wa habari,)”

“Lakini changamoto kubwa ambayo naiona DRFA ni kwamba chama hiki  kinafanya mambo mengi makubwa sana lakini mambo hayo hayasikiki kwa upana wake, kwa hiyo kwa nafasi hii ambayo nimepewa,nitahakikisha nayafikisha kwa wananchi” alifafanua Katanga.

Comments are closed.