KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, UTALII, UTAMADUNI NA MICHEZO WA SERIKALI YA MAPINDUZI AAHIDI KUTOA HUDUMA BORA

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, UTALII, UTAMADUNI NA MICHEZO WA SERIKALI YA MAPINDUZI AAHIDI KUTOA HUDUMA BORA

Like
267
0
Friday, 22 April 2016
Local News

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Hassan Omar amesema atahakikisha anasimamia na kutekeleza adhima ya Serikali hiyo ya kuwapatia wafanyakazi wake huduma bora ili waweze kutekeleza kazi zao kwa ufanisi.

Mheshimiwa Omar Hassan Omar ameyasema hayo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na Katibu mkuu aliyemaliza muda wake Ali Mwinyikai katika ukumbi wa Wizara iliyopo Mnazi mmoja visiwani.

Amesema utendaji kazi wa Serikali ni wa pamoja  na sio mtu mmoja mmoja hivyo amewaomba viongozi na wafanyakazi wa wizara kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.

 

Comments are closed.