KATUMBI ATANGAZA KUWANIA URAIS CONGO

KATUMBI ATANGAZA KUWANIA URAIS CONGO

Like
264
0
Thursday, 05 May 2016
Global News

MWANASIASA mashuhuri wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.

Mfanyabiashara huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga ametoa tangazo hilo kupitia mitandao ya kijamii.

Muungano wa vyama kadhaa vya upinzani nchini humo umeamua kumuidhinisha Bwana Katumbi kuwa mgombea wao wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi huo.

Comments are closed.