UMOJA wa Mataifa umesema ubakaji na njia nyingine za matumizi ya nguvu yanafanywa na pande zote katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan kusini.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya nguvu kingono katika mizozo ya kivita, Zainab Hawa Bangura, amesema hali hiyo imesambaa mno ambapo hadi mtoto wa miaka miwili alikuwa miongoni mwa wahanga.
Mapigano yalizuka Desemba mwaka jana nchini Sudan kusini baada ya miezi ya hali ya wasiwasi kati ya rais Salva Kiir, na hasimu wake kisiasa Riek Machar.