KAULI YA UN KUHUSU MATUMIZI YA NGUVU KINGONO SUDANI KUSINI

KAULI YA UN KUHUSU MATUMIZI YA NGUVU KINGONO SUDANI KUSINI

Like
297
0
Tuesday, 21 October 2014
Global News

UMOJA wa  Mataifa  umesema  ubakaji  na  njia  nyingine za matumizi  ya  nguvu yanafanywa  na  pande  zote katika  vita vya  wenyewe  kwa  wenyewe  nchini  Sudan  kusini.

Mwakilishi maalumu  wa  Umoja  wa  Mataifa  kuhusu  matumizi  ya  nguvu kingono katika  mizozo  ya  kivita, Zainab Hawa  Bangura, amesema hali  hiyo  imesambaa  mno  ambapo  hadi  mtoto  wa  miaka  miwili alikuwa  miongoni  mwa  wahanga.

Mapigano  yalizuka Desemba mwaka  jana  nchini  Sudan kusini baada  ya  miezi ya  hali  ya wasiwasi  kati  ya  rais Salva Kiir, na  hasimu  wake  kisiasa  Riek Machar.

 

Comments are closed.