KENYA: MAHAKAMA YASIMAMISHA MGOMO WA WAALIMU

KENYA: MAHAKAMA YASIMAMISHA MGOMO WA WAALIMU

Like
227
0
Friday, 25 September 2015
Global News

MAHAKAMA nchini Kenya imesimamisha mgomo wa walimu uliodumu kwa wiki nne na kuwaagiza walimu kurudi kazini mara moja.

 

Jaji Nelson Abuodha wa mahakama ya kiviwanda na masuala ya wafanyakazi amesimamisha mgomo huo kwa miezi mitatu na kuwataka walimu na serikali kuunda kamati ya kutafuta suluhu katika muda wa mwezi mmoja.

 

Aidha, ameiagiza Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) kutowaadhibu walimu na kuwalipa mishahara yao kikamilifu, pamoja na marupurupu.

Comments are closed.