KENYA: ORSBONE MONDAY ATEKWA NYARA

KENYA: ORSBONE MONDAY ATEKWA NYARA

Like
250
0
Thursday, 13 August 2015
Slider

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Orsbone Monday amepotea baaada ya kuchukuliwa na watu wasio julikana huku wakijitambulisha kwao kuwa ni maafisa wa polisi.

Mchezaji wa timu ya Tusker FC ya Kenya ameripotiwa kupotea huku taarifa zaidi zikieleza kuwa ametekwa nyara na watu wasiojulikana.

Mama mzazi wa Orsbone ameripotiwa akiesema kwamba mtoto wake alifuatwa nyumbani kwake na watu 10 wasiojulikana ambao walijitambulisha kuwa ni polisi kutoka kituo cha Kenyatta ambao hawakuruhusu namba za magari waliyoenda nayo kuchukuliwa na mama mzazi wa mchezaji huyo pamoja na mwanae na baadae kumfahamisha kwamba iwapo mama huyo atahitaji kumuona mwanae afike kwenye kituo hicho cha polisi.

Lakini kinyume na matarajio mama huyu alipofika kituoni hapo hakukuta taarifa za mwanae hali iliyomfanya azunguke katika vituo mbalimbali akimtafuta mchezaji huyo bila mafanikio.

Tusker FC kwa upande wao pia wameripoti taarifa hiyo kwenye ukurasa wao wa facebook juu ya kupotea kwa mchezaji huyo

Comments are closed.