SERIKALI ya Kenya imeagiza shule zote nchini humo zifungwe kuanzia Jumatatu ijayo huku mgomo wa walimu ukiendelea.
Barua iliyotolewa na wizara ya elimu nchini humo imeagiza shule zote za umma na binafsi zifungwe na wanafunzi warudi nyumbani na kwamba watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kwa Katibu Mkuu wa chama cha walimu nchini humo KNUT zinasema kuwa tayari amepokea barua hiyo ya kufungwa kwa shule kutoka serikalini.