WAKENYA wameandamana kudai usalama zaidi wa taifa hilo kufuatia mauaji ya wiki iliyopita yaliyofanywa na wapiganaji kutoka Somalia wa kundi la Al-Shabaab , kabla ya kuwasha mishumaa usiku katika siku ya mwisho ya Maombolezi kutokana na kuuwawa kwa watu 148 mjini Garissa.
Ndege za kivita za Kenya zimeshambulia maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo lenye mafungamano na Al-Qaeda Kusini mwa Somalia , lakini hasira imekuwa ikiongezeka kuhusiana na madai kwamba onyo muhimu la kijasusi lilipuuzwa.
Vikosi maalum vya jeshi vimechukua Saa saba kufika katika Chuo Kikuu cha Garissa, kilometa 365 kutoka Mji Mkuu Nairobi , wakati wapiganaji wa Al-Shabaab walipovamia Mabweni ya Wanafunzi na kuanza kuwauwa.