KENYA YAAHIDI KUSAMEHE RAIA WAKE WALIOPOKEA MAFUNZO YA KIGAIDI WATAKAOJISALIMISHA NDANI YA SIKU KUMI ZIJAZO

KENYA YAAHIDI KUSAMEHE RAIA WAKE WALIOPOKEA MAFUNZO YA KIGAIDI WATAKAOJISALIMISHA NDANI YA SIKU KUMI ZIJAZO

Like
202
0
Wednesday, 15 April 2015
Global News

SERIKALI ya Kenya imeahidi kuwasamehe wakenya ambao wamepokea mafunzo ya kigaidi endapo watajitokeza katika kipindi cha siku 10 zijazo.

Waziri wa Usalama wa Mambo ya Ndani, Jenerali mstaafu Joseph Nkaissery ambae pia amewaonya wazazi wa vijana kama hao kwamba watachukuliwa hatua kali endapo hawataijulisha serikali kuhusu kujiunga kwa wanao na kundi la Al Shabaab.

Serikali imewapa wale wote waliopokea mafunzo kutoka kwa Al Shabaab siku kumi kujisalimisha katika ofisi za wasimamizi wa miji ya Garissa, Mombasa au Nairobi.

 

Comments are closed.