KENYA YAASWA KUTOFUNGA KAMBI ZA WAKIMBIZI

KENYA YAASWA KUTOFUNGA KAMBI ZA WAKIMBIZI

Like
279
0
Tuesday, 10 May 2016
Global News

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR limeitaka serikali ya Kenya kubatilisha msimamo wake wa kutaka kuzifunga kambi mbili za wakimbizi ikiwemo ya Dadaab nchini humo.

Awali siku ya Ijumaa iliyopita Serikali ya Kenya ilisema kwamba kambi hizo mbili zitafungwa kufuatia wasiwasi wa usalama na ukosefu wa fedha.

Aidha imetoa tangazo kama hilo mapema, lakini wakati huu serikali imesema kuwa inazifunga kambi zake za wakimbizi katika kile kinachoonekana kama hatua ya kwanza ya kusitisha uhifadhi wa wakimbizi Laki sita.

Comments are closed.