KENYATA KUTEMBELEA WANAJESHI WALIOJERUHIWA NA AL-SHABAB

KENYATA KUTEMBELEA WANAJESHI WALIOJERUHIWA NA AL-SHABAB

Like
318
0
Friday, 22 January 2016
Global News

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajia kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa baada ya wanamgambo wa Al-Shabab kushambulia kambi ya wanajeshi nchini Somalia Ijumaa iliyopita.

Rais Kenyatta atawatembelea majeruhi hao katika hospitali ya Forces Memorial iliyopo Nairobi na baadaye kujumuika na ndugu, marafiki na maafisa wakuu wa Jeshi kwa ibada ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa.

Serikali ya Kenya bado haijatoa idadi kamili ya wanajeshi wake waliouawa baada ya kambi hiyo iliyoko El-Ade kushambuliwa ingawa Mkuu wa Majeshi nchini humo Jenerali Samson Mwathethe amewaambia wanahabari jana kuwa jeshi bado linaendelea kufanya uchunguzi kuhusu wanajeshi waliokuwa kwenye kambi hiyo.

Comments are closed.