KERRY AFUNGUA SIKU YA PILI YA MAZUNGUMZO MJINI GENEVA

KERRY AFUNGUA SIKU YA PILI YA MAZUNGUMZO MJINI GENEVA

Like
229
0
Monday, 02 May 2016
Global News

WAZIRI wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry amefungua siku ya pili ya mazungumzo mjini Geneva yenye lengo la kutafuta njia  ya kupata suluhu ya mapigano nchini Syria.

Kerry  amekutana na Waziri wa  mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia  Adel Al-Jubeir na anapanga pia kuwa na mazungumzo baadae na  mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Syria Staffan De Mistura.

Waziri Kerry amesema hatua za maelewano kuhusu njia ya kupunguza mashambulizi mjini Aleppo zinaendelea kuimarika, lakini kazi ya ziada inahitajika.

Comments are closed.