KERRY NA PUTIN KUIJADILI SYRIA

KERRY NA PUTIN KUIJADILI SYRIA

Like
156
0
Tuesday, 15 December 2015
Global News

WAZIRI wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry yupo nchini Moscow kwa ajili ya mazungumzo na Rais Vladimir Putin kuhusu njia za kumaliza vita vinavyoendelea nchini Syria.

Mazungumzo hayo yanalenga kupunguza mfarakano kati ya Urusi na Marekani, hasa kuhusu makundi ambayo yanafaa kujumuishwa kwenye mazungumzo ya mzozo huo.

Urusi ambayo inamuunga mkono Rais wa Syria Bashar Al-Assad, imesema mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita wa makundi yanayopinga serikali ya Syria haukuwakilisha makundi yote yanayovutana katika mzozo huo.

Comments are closed.