KESHI AREJEA KUINOA SUPER EAGLES

KESHI AREJEA KUINOA SUPER EAGLES

Like
245
0
Friday, 27 March 2015
Slider

Rais wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF bwana Amaju Pinnick amethibitisha kufanyika kwa mazungumzo na kukubaliana na kocha Stephen Keshi kurejea kuinoa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 anahistoria ya kuiongoza Super Eagles kutinga raundi ya pili ya kombe la dunia lililofanyika mwaka jana.

Keshi amekuwa na kikosi hikcho tangu mwaka 2011 na kuacha kukitumikia alipotoka nchini brazili kwa madai ya kuwa amepata mkataba mwingine.

Hata hivyo mzozo katika shirikisho la mpira wa miguu Nigeria ulilazimu mazungumzo na kocha huyo kuendelea kwa kipindi kirefu hadi hivi sasa ambapo wamefikia makubaliano na kocha huyo kuinoa Super Eagles kwa miaka miwili

Keshi anakumbukwa kwa ushindi wa kombe la mataifa ya Afrika katika awamu yake ya kwanza mwaka wa 2013.

”Sote kama kamati tumekaa na kukubaliana kuwa Keshi anastahili kuendelea na majukumu yake katika timu ya taifa”

”Naamina kuwa ataweka sahihi karibuni na kuanza kazi” alisema Pinnick.

 

 

 

Comments are closed.