KESI YA HABRE KUANZA LEO

KESI YA HABRE KUANZA LEO

Like
283
0
Monday, 07 September 2015
Global News

KESI inayomkabili aliyekuwa rais wa Chad, Hissène Habré dhidi ya uhalifu kwa binadamu, kivita na mateso, inaanza kusikilizwa leo

Jaji wa mahakama ya Burkinabe, Gberdao Gustave Kam ataamua iwapo kesi hiyo itaendelea bila upande wa utetezi wa Hissene Habre.

Tangu mwanzo wa utaratibu wa kesi hiyo, Hissene Habre, mwenye umri wa miaka 72 amekuwa akikataa kutambua uhalali wa mahakama maalum ya Afrika, ambayo iliundwa na Umoja wa Afrika mwaka 2013, ili kushugulikia kesi yake nchini Senegal.

Comments are closed.