KAMPUNI ya Kidoti inayojishughulisha na utengenezaji wa Nywele, Viatu, Mikoba na bidhaa mbalimbali leo imesaini mkataba wa dolla milioni tano kwa lengo la kujenga Ushirikiano na Kampuni ya Rainbow shell Craft ya Nchini China.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kidoti, Jokate Mwegelo amesema ubia huo unalengo la kuiwezesha Kampuni ya Kidoti kuweza kupanua wigo wake kibiashara ikilenga pia kujiweka zaidi katika soko la Afrika Mashariki, Kati na Duniani.
Amesema Kampuni hiyo ya China iliyowekeza nchini Tanzania katika Sekta ya Kilimo na kujishughulisha na mitindo mbalimbali ya nywele na bidhaa zingine, imedhamiria kuhakikisha kuwa Kidoti na timu yake wanajifunza kutoka kwao ili kujikwamua kiuchumi na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Rainbow and Shell Craft Deng Liuoxun, amesema ushirikiano huo utasaidia kuongeza uwezo wa Vijana katika kampuni ya Kidoti, kujikwamua Kiuchumi kwakutengeneza bidhaa zao wenyewe.