KIFAA CHA KUNASA SAUTI KWENYE NDEGE UJERUMANI CHAHARIBIKA

KIFAA CHA KUNASA SAUTI KWENYE NDEGE UJERUMANI CHAHARIBIKA

Like
290
0
Wednesday, 25 March 2015
Global News

WAZIRI wa maswala ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve, amesema kuwa kifaa cha kunasa sauti kwenye ndege kilichopatikana hapo jana Jumanne baada ya kuanguka kwa  ndege ya Ujerumani katika milima ya Alps kimeharibika.

Hata hivyo amesema kuwa kifaa hicho bado kitatoa taarifa kwa watalamu wanaojaribu kubaini kilicho sababisha kuanguka kwa ndege hiyo, ambayo iliwauwa abiria wote 150 na wahudumu waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

Shughuli za utafutaji wa ndege hiyo zimeendelea huku helikopta zinaonekana zikipaa katika maeneo hayo na maafisa wa polisi wameendelea kuchunguza mabaki ya ndege .

 

Comments are closed.