KIKOSI MAALUM CHA JESHI LA IRAQ KIMEFANYA MASHAMBULIZI DHIDI YA IS

KIKOSI MAALUM CHA JESHI LA IRAQ KIMEFANYA MASHAMBULIZI DHIDI YA IS

Like
240
0
Wednesday, 23 December 2015
Global News

KIKOSI maalumu cha jeshi la Iraq cha kupambana na ugaidi kimeingia katikati mwa mji wa Ramadi unaodhibitiwa na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la Dola la Kiislamu IS

Msemaji wa jeshi Sabah al Numani, amesema kikosi hicho maalumu hakikukumbana na upinzani mkali isipokuwa mashambulizi machache kutoka kwa washambuliaji wa kujitoa muhanga katika juhudi za kuukomboa mji huo mkuu wa jimbo la Anbar kutoka kwa IS.

Taarifa za kiusalama zinaarifu kuwa huenda kuna kati ya wanamgambo 250 hadi 300 wa IS wanaosalia katika mji huo..

Comments are closed.