KILELE CHA MAZUNGUMZO JUU YA MGOGORO WA UKRAINE KUFIKIWA HIVI KARIBUNI

KILELE CHA MAZUNGUMZO JUU YA MGOGORO WA UKRAINE KUFIKIWA HIVI KARIBUNI

Like
266
0
Friday, 13 February 2015
Global News

MSEMAJI wa Ikulu Nchini Urusi amesema leo hii kwamba viongozi wa Urusi,Ukraine na Ujerumani wanaendelea kuwasiliana juu ya suala la mzozo wa Ukraine na kwamba anatarajia mazumgumzo hayo kwa njia ya simu yatafikiwa siku chache zijazo.

Dmitry Peskov amesema serikali ya Urusi inatarajia vipengele vyote vilivyomo katika makubaliano ya kusitisha mapigano yaliofikiwa Minsk vitatekelezwa.

Usitishaji wa mapigano katika eneo zima la  mzozo unatakiwa uanze Jumapili ambapo pande zote mbili zinatakiwa zianze kuondowa silaha nzito kutoka kwenye medani ya mapambano katika kipindi kisichozidi siku mbili.

 

Comments are closed.