KIM JONG UN AAMURU MAJESHI KUKAA TAYARI KWA VITA

KIM JONG UN AAMURU MAJESHI KUKAA TAYARI KWA VITA

Like
363
0
Friday, 21 August 2015
Global News

KIONGOZI wa  Korea kaskazini  Kim Jong-Un ameamuru  majeshi yaliyoko mstari  wa  mbele  kuwa tayari  kwa  vita  leo, wakati  hali  ya  wasi wasi ya kijeshi  na  Korea kusini  ikiongezeka.

Hali hiyo inafuatia  mashambulizi ya  makombora toka  kila  upande  katika  eneo  lenye  silaha  nzito  la  mpakani.

Shirika rasmi  la habari  la  Korea  kaskazini KCNA limesema  hatua  hiyo  imekuja wakati  wa  mkutano  wa  dharura uliofanyika jana  usiku wa  kamisheni  kuu yenye madaraka  makubwa  ya   kijeshi ambapo  Kim ndie  mwenyekiti  wake.

Comments are closed.