KIMBUNGA kilichokuwa na kasi ya kilometa 200 kwa saa kimeukumba mji wa Sydney nchini Australia leo , na kuezuwa mapaa ya nyumba katika kitongoji cha kusini ya pwani ya mji huo na kusababisha mafuriko na mvua ya mawe.
Kimbunga hicho , kilichokuwa na upepo mkali kuwahi kuonekana katika mji wa Sydney , kilikuwa sehemu ya kimbunga kikubwa kilicholikumba eneo la pwani ya kusini ya New South Wales na Sydney kabla ya kuelekea upande wa kaskazini, na kusababisha mafuriko na uharibifu mkubwa wa mali.