KINANA: WAMASAI NI WATANZANIA HALALI

KINANA: WAMASAI NI WATANZANIA HALALI

Like
974
0
Thursday, 18 December 2014
Local News

KATIBU MKUU wa Chama Cha Mapinduzi-CCM ABDULRAHMAN KINANA amesema kuwa watu wa Kabila la Wamasai ni watanzania halali na kwamba hawana sababu ya kutafuta Uraia kwenye Maeneo mengine.

Kinana ameeleza kuwa tatizo la migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na Wafugaji kuingia kwenye mapori ya Akiba na Hifadhi za Taifa haliwahusu Wamasai pekee bali ni la nchi nzima.

Kiongozi huyo wa chama cha Mapinduzi, ametoa kauli hiyo wakati akijibu Malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa Mila wa Kabila la Wamasai katika Semina ya masuala ya ardhi inayofanyika Namanga Wilayani Longido mkoani Arusha.

 

Comments are closed.