KINGUNGE: MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS CCM ULIKUWA BATILI

KINGUNGE: MCHAKATO WA KUMPATA MGOMBEA URAIS CCM ULIKUWA BATILI

Like
237
0
Wednesday, 15 July 2015
Local News

MWANASIASA Mkongwe na Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi- CCM -Kingunge Ngombale Mwiru ameeleza kusikitishwa kwake na mchakato mzima wa kumpata Mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho kuwa ulikua ni batili na kulikua na ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama hicho.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipozungumza na Waandishi wa habari, ambapo amesema kwa Mujibu wa Taratibu za Chama hicho Kamati kuu ndio yenye jukumu la kuteua Tano bora katika wanachama wote waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo jambo ambalo halikufanyika.

Kingunge amesema Kamati hiyo ya Maadili imewakosesha wagombea kupita mbele ya kamati kuu kujieleza na imewanyima wajumbe wa kamati kuu kuteua tano bora jambo ambalo pia limewanyima Watanzania Mgombea wanaempenda ambae ni Edward Lowasa.

 

Comments are closed.