KINSHASA: MAMIA YA WATU WAKUSANYIKA KUUPOKEA MWILI WA PAPA WEMBA

KINSHASA: MAMIA YA WATU WAKUSANYIKA KUUPOKEA MWILI WA PAPA WEMBA

Like
333
0
Thursday, 28 April 2016
Global News

MAMIA ya watu wamekusanyika nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan.

Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho.

Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Comments are closed.