KIONGOZI MASHUHURI WA SINGAPORE AFARIKI DUNIA

KIONGOZI MASHUHURI WA SINGAPORE AFARIKI DUNIA

Like
298
0
Monday, 23 March 2015
Global News

KIONGOZI  mashuhuri  wa  Singapore, anayejulikama  kama  baba  wa taifa  hilo , Lee Kuan Yew  amefariki dunia.

Serikali  ya  nchi  hiyo imetangaza  hii  leo kwamba  Lee  mwenye  umri  wa  miaka  91 alilazwa  hospitalini  mapema  Februari  akiwa  anaugua  ugonjwa wa  kichomi, na  amekuwa  akipumua  kwa  kutumia  mashine  katika kitengo  cha  wagonjwa  mahututi  tangu wakati  huo.

Rais  wa  Marekani  Barack Obama  ametuma salamu  zake  za rambi rambi  na  kumuelezea  Lee  kuwa  mtu  aliyeona  mbali. Nae katibu  mkuu  wa  Umoja  wa  Mataifa  Ban Ki-moon  amesema amesikitishwa  mno  na  kifo  cha  Lee , na  kusema  alikuwa  mtu muhimu  katika  bara  la  Asia.

 

Comments are closed.