KIONGOZI WA DA ATANGAZA KUTOGOMBEA TENA UCHAGUZI UJAO

KIONGOZI WA DA ATANGAZA KUTOGOMBEA TENA UCHAGUZI UJAO

Like
246
0
Monday, 13 April 2015
Global News

KIONGOZI wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance, DA, amesema hatagombea katika uchaguzi wa chama hicho mwezi ujao.

Helen Zille amesema ni wakati muafaka kwake kutogombea, akisema kuwa DA watanufaika na mchango wa vijana.

Atabaki kuwa waziri mkuu wa jimbo la Western Cape hadi mwaka 2019.   Zille, ni mwandishi wa habari wa zamani na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi amekiongoza chama hicho tangu mwaka 2007.

Comments are closed.