Kiongozi wa upinzani nchini Bahrain ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Kiongozi wa upinzani nchini Bahrain ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Like
514
0
Monday, 05 November 2018
Global News

Kiongozi wa upinzani nchini Bahrain Sheikh Ali Salman amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufaa kumpata na hatia ya kupeleleza kwa niaba ya Qatar.

Hukumu hiyo inakuja miezi michache baada ya mahakama ya juu nchini Bahrain kumuondolea mashtaka Salman kwa kushirikiana na taifa hasimu.

Bahrain ilikata uhusiano wake na Qatar mwaka 2017.

Shirika la haki za binadamu la Amnesty limetaja uamuzi huo kama ukiukaji wa haki wakati huu Bahrain inaendelea kuwazima wakosoaji.

Ali Salman ambaye aliongoza vuguvugu ambalo sasa limepigwa marufuku la Al-Wefaq, alilaumiwa kwa kushirikiana na Qatar kue

Wawili hao hawajahukumiwa vifungo vya maisha.

Kwa nini sasa?

Mwendesha mashtaka nchini Bahrain alisema wanaume hao watatu walifungwa kwa kuwasiliana na maafisa wa Qatar kuipindua serikali.

mwendesha vurugu dhidi ya serikali mwaka 2011 pamoja na viongozi wenzake wa upanzani Hassan Sultan na Ali al-Aswad.

Lakini madai hayo ambayo ni ya miaka saba iliyopita yalifichuliwa mwaka uliopita baada ya Bahrain, Saudi Arabia, UAE na Misri kukata uhusiano na Qatar.

Washirika hao waliilaumu Qatar kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi na kuwa karibu sana na Iran, madai ambayo Qatar inayakana.

Kipi kilifanyika mwaka 2011?

Waandamanaji wakiongozwa na jamii kubwa ya Shia waliingia barabarani Februari mwaka 2011 wakitaka demokrasia ziaid.

Lakini familia ya kifalme ya Al Khlifa inayoshikilia nafasi nyingi za kisiasa na kijeshi ilizima maandamano hayo kwa msaada ya nchi majirani hasa Saudi Arabia.

Ghasia hizo zilisababisha vifo vya watu 30 wakiemo polisi 5.

Tangu wakati huo Bahrain imekumbwa na misukosuko. Kujibu, Bahrain imepiga marufuku vikundi vya upinzani huku mamia ya wakosoaji wa serikali wakifungwa.

 

 

cc;BBCswahili

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *